Kwa mtazamo wa Tanzania nzima, magari yaliyopo sokoni huanzia takribani TSh 3M kwa magari madogo ya matumizi ya kila siku na kufika hadi TSh 750M kwa SUV kubwa, 4x4 na magari ya kifahari ya kiwango cha showroom.
Magari tunayoyaona sokoni huwa ya miaka mbalimbali, kuanzia takribani 1994 hadi 2025, na wastani wa bei ukiwa TSh 53.2M. Magari used ya miaka ya nyuma huwa nafuu zaidi, wakati magari ya miaka mipya, yenye mileage ndogo na yaliyokaribia ubora wa magari ya showroom bei huwa juu zaidi.
Pia aina ya usajili wa plate namba ya gari una athari kubwa kwenye bei. Magari ambayo hayajasajiliwa lakini ushuru wote umelipwa mara nyingi huwa na bei ya juu zaidi, karibu sawa na bei za gari hii showroom Dar es salaam. Magari yenye namba kama Namba E, D, C, B au A huwa bei nafuu, na kadiri herufi inavyoshuka (kwa mfano kutoka E kwenda A) ndivyo bei za magari inavyopungua.
Badala ya kutegemea showroom moja au maelezo ya muuzaji mmoja pekee, tumia GariPesa kulinganisha magari used na magari yaliyo karibu na kiwango cha showroom kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, ili ufanye maamuzi ya bei kwa ujasiri zaidi.
GariPesa ni soko la mtandaoni la magari linalokuunganisha moja kwa moja na wauzaji na wanunuzi nchini Tanzania. Unaweza kutafuta magari kwa Make, Model, Mkoa, bei na vigezo vingine, kisha kuwasiliana na muuzaji kupitia simu au WhatsApp.
Kabla ya kuamua kununua, hakikisha unakagua gari kwa macho, kufanyiwa ukaguzi na fundi, kuangalia historia ya matengenezo na nyaraka kama kadi ya gari na mkataba sahihi. Epuka kutuma pesa bila kumwona muuzaji ana kwa ana kwenye eneo salama.
Kwa sasa GariPesa ni jukwaa la matangazo na halishiki fedha kwa niaba ya wanunuzi au wauzaji. Malipo hufanyika moja kwa moja kati ya pande mbili. Tunashauri kila upande kufuata taratibu za usalama, mikataba iliyoandikwa na kukutana maeneo salama.
Epuka ofa ambazo zinaonekana nzuri sana kuliko kawaida, usitume pesa bila kuliona gari na kumbukumbu kamili, na usikubali kushawishiwa kukutana maeneo hatarishi. Tumia mawasiliano rasmi na uhakikishe jina kwenye malipo linaendana na maelezo ya muuzaji.
Ndiyo, unaweza kutumia vichujio kama bei ya chini na ya juu, mwaka wa uzalishaji, hali ya gari na Mkoa ili kuona magari yanayolingana na bajeti na mahitaji yako. Unaweza pia kulinganisha matangazo kadhaa ya modeli moja kabla ya kuamua.