Kuna sababu mbalimbali zinazopelekea mtu kuamua kuuza gari lake na hizi zote ndio zinaweza kusaidia katika kupanga bei ya kuuza lakin kama huyo mtu anauza gari kwa shida au mahitaji binafsi nayo pia uchangia katika kupanga bei ya kuiuza kutokana na uharaka wa uhitaji wake. Unapofikia hatua ya kuuza gari lako, jambo la kwanza la kuzingatia ni bei sahihi. Bei isiyo sahihi inaweza kusababisha gari lako kukaa sokoni kwa muda mrefu au kukuuza kwa hasara. Tanzania ina soko la magari linaloendeshwa na hali ya uchumi, mahitaji ya watumiaji, na upatikanaji wa vipuri, hivyo ni muhimu kuelewa vigezo muhimu kabla ya kuweka bei.
- Tambua Aina ya Gari na Umaarufu Wake Sokoni
Magari maarufu kama Mazda Demio, Toyota Vitz, Harrier, RAV4, Toyota IST, Mazda Verisa, Nissan X-Trail, au Toyota Alphard huwa na soko la haraka kutokana na urahisi wa vipuri na matumizi madogo ya mafuta. Kama gari lako ni moja ya haya, unaweza kuweka bei ya ushindani. Kwa magari yasiyo ya kawaida au ya kifahari kama BMW au Mercedes-Benz, weka bei kwa kuzingatia idadi ndogo ya wanunuzi na gharama kubwa za matengenezo. - Angalia Hali ya Gari (Ubora wake)
Je, gari lina matatizo ya injini, umeme, au lina mwonekano mzuri? Magari yaliyotunzwa vizuri hupata bei ya juu kutokana na kutunzwa kwake. Elezea wazi hali ya gari kwa ujumla kama vile tairi, service record, mileage (km ngapi limekwenda), na kama limewahi kupata ajali. Wauzaji wengi wa magari wamekuwa wanaficha baadhi ya taarifa kwaajili ya kuogopa kuuza gari kwa bei ya hasara lakini sisi garipesa taarifa zote tunaziweka wazi kipindi unapotaka kununua gari kutoka kwetu. Gari lenye matunzo ya mara kwa mara linaweza kuuzwa kwa bei ya juu zaidi. - Fanya Utafiti wa Soko
Unapotaka kupanga bei tembelea tovuti na kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii kuangalia bei ya magari ya aina yako unayotaka kuuza lakini pia unaweza kutembelea sehemu wanazouza magari na kufanya tafiti za bei hii utakusaidi sana kupanga bei kulingana na hali ya gari lako. Tafuta magari ya aina kama yako, ya mwaka sawa na hali inayofanana. Angalia bei wanazouza watu wengine, kisha tumia wastani huo kama mwongozo. - Zingatia Mwaka wa Kutengenezwa (Model Year)
Magari mapya au ambayo bado hayajasajiliwa hapa kwetu Tanzania yana bei ya juu zaidi. Lakini, gari la mwaka wa zamani linalotunzwa vizuri linaweza kuvutia wanunuzi wa bajeti ndogo na hata bajeti kubwa kutoka na uhitaji na chaguo la mteja. Epuka kuweka bei ya juu kwa gari lililotumika kwa miaka mingi bila sababu ya msingi. - Gharama za Kuagiza na Kodi
Weka akilini kuwa watu wengi wanapopanga kununua gari, hulinganisha na gharama za kuagiza moja kwa moja kutoka Japani, UAE au UK. Kwa hiyo, kama bei yako iko juu kuliko ya kuagiza na kulipia kodi zote, kuna uwezekano mkubwa usipate mteja. - Upatikanaji wa Vipuri na Utaalamu wa Mafundi
Magari ambayo vipuri vyake ni vigumu kupatikana au vinavyohitaji mafundi wa kitaalamu na ulaji mkubwa wa mafuta huwa na thamani ya chini sokoni na pengine kuchelewa kuuzika. Ukigundua kuwa gari lako ni miongoni mwa haya, zingatia kushusha bei kidogo ili kuvutia wanunuzi. - Muda wa Kuliuza Gari
Kama unahitaji kuuza gari haraka, uwe tayari kushusha bei. Ikiwa una muda wa kusubiri, unaweza kuanza na bei ya juu kisha kupunguza taratibu kadri siku zinavyokwenda. - Tumia Majaribio ya Bei (Negotiation Room)
Weka bei ambayo ina nafasi ya kushusha kidogo kwa mnunuzi atakayependa kuzungumza kuhusiana na bei. Mfano, kama unataka Sh 14,000,000, weka bei ya awali kuwa Sh 15,000,000 ili wateja wapate nafasi ya kujadiliana bila kupunguza thamani yako halisi.
Hitimisho
Bei sahihi ya gari ni ile inayozingatia hali ya soko, ubora wa gari lako, na ushindani uliopo. Kwa kufanya utafiti wa kina, kuelewa thamani ya gari lako, na kuwa mkweli kuhusu hali yake, utaweza kuvutia wanunuzi sahihi na kuuza kwa haraka bila hasara. Usisahau kuwa tayari kwa mazungumzo ya bei na kuwa na nyaraka zote muhimu tayari (kama kadi ya gari na namba ya mauzo).Karibu garipesa kwaajili ya kujipatia magari yenye ubora wa hali ya juu na bei rafiki kwa kipato cha Mtanzania