Unapotaka kuuza gari lako tegemea kupokea simu au ujumbe kutoka kwa wanunuzi je waje kukagua gari au waachane nalo. Wengi wao watakuuliza maswali yanayofanana kuhusu hali ya gari, bei na sababu ya kuuza. Hapa chini ni baadhi ya maswali ya kawaida na jinsi bora ya kuyajibu ili kuvutia mnunuzi bila kupoteza uaminifu.
1. “Kwa nini unauza gari?”
Hili ni swali la kwanza linaloulizwa na wateja wengi.
Jibu bora: Jibu kwa uaminifu lakini kwa njia chanya. Mfano:
- “Ninauza kwa sababu ninahitaji kubadilisha gari.”
- “Ninauza kwasababu nina shida nataka kutatua .”
Epuka majibu kama: “Gari lina matatizo sana” hata kama kuna kasoro ndogo, unaweza kusema “Kama kuna kasoro, ni ndogo na zinaweza kurekebishwa kwa urahisi.”
2. “Gari lina vipengele vyovyote?”
Wanunuzi wanataka uhakika kuwa hawataingia gharama kubwa baada ya kununua.
Jibu bora:
- “Gari lipo kwenye hali nzuri, service zote zimefanyika kwa wakati. Kuna kasoro ndogo kama XXX lakini si jambo kubwa.”
- Ikiwa hakuna matatizo makubwa, unaweza kusema: “Kwa sasa halina matatizo yoyote makubwa yanayohitaji matengenezo.”
3. “Je Limeshawahi kupata ajali?”
Wanunuzi wengi wanaogopa magari yaliyowahi kupata ajali kubwa.
Jibu bora:
- Gari hili halijawahi kupata ajali yoyote ile
- “Gari halijawahi kupata ajali kubwa. Kama kuna scratch ndogo au dent, ni ya kawaida ya matumizi ya kila siku.” jibu hili ni kama lilishawahi kupata ajali
- Ikiwa liliwahi kupata ajali, sema ukweli lakini eleza kuwa tayari lilisharekebishwa kikamilifu.
4. “Imetembea ni kilomita ngapi?”
Wanunuzi wengi hupendelea hili swali kwaajili ya kutaka kujua kama gari imetumiwa sana au laah
Jibu bora:
Toa Kilomita halisi inayoonekana kwenye dashboard na uongezee:
- “Kwa Kilomita hizi, gari bado lipo kwenye hali nzuri na service zote zimekuwa zikifanyika kwa wakati.”
- Kama Kilomita ni nyingi, eleza historia ya matengenezo kama engine overhaul au service kubwa zilizowahi kufanyika.
5. “Gari lina document zote na Wewe ndio Mmiliki?”
Hili ni swali muhimu sana linahusu umiliki halali wa gari.
Jibu bora:
- “Ndio, gari lina kadi ya usajili wenye jina langu. Hili ni kwa yule anayeuza gari lake ambalo kadi ya gari inasoma jina lake
- Ndio, gari lina kadi ya gari pamoja na faili lote lakini kadi ya gari haisomi jina langu kwasababu niliponunua sikuweza kubadilisha umiliki lakini mkataba wa mauziano ninao
- Kama kuna kitu bado kipo kwenye mchakato, eleza wazi.
6. “Bei ni ya mwisho ni ngapi?”
Wateja wengi hupenda kupunguziwa bei na hata kabla hajaja kuliona gari basi hupenda kuuliza bei ya mwisho ni kiasi gani au je bei hio uliyotaja inapungua?
Jibu bora:
- “Bei niliyoweka ni ya maelewano kidogo kwa mnunuzi mwenye nia ya kweli.”
- Au: “Ni fixed kwa sasa kutokana na hali nzuri ya gari, lakini kama utakuja kuliona, tunaweza kuongea kidogo.”
7. “Je limeshawahi kurudiwa rangi?”
Wateja wengi hupendelea hili swali kwaajili ya kutaka kujua sababu kwanini gari imerudiwa rangi kama gari litakuwa limerudiwa rangi kusudi kuona kama liliwahi kupata ajali au lah
Jibu bora:
- “Gari hili halijawahi kurudiwa rangi mahala popte pale” Jibu hili ni kwa gari ambalo halijawahi kabisa kurudiwa rangi
- Gari hili limewahi kurudiwa rangi kwenye bampa tu la mbele kutokana na kuwa lilikwaruzika sana kutokana na hali zetu za barabara na gari kuwa chini “ Jibu hili kwa gari zilizo chini
- Au gari hili halijawahi kurudiwa rangi ila limewahi kupigwa polishi gari nzima kutokana na rangi yake kuwa imefubaa kutokana na jua
Hitimisho
Kuwa mkweli lakini pia jitahidi kuweka majibu yako kwenye lugha chanya. Epuka kutoa majibu ya kukatisha tamaa au yasiyoeleweka. Wanunuzi wanapenda wauzaji wa wazi, waaminifu na wanaojibu maswali kwa haraka. Hii huongeza nafasi yako ya kufunga dili haraka!