Kuuza au kununua gari kunahitaji umakini ambao utakusaidia kuepuka changamoto nyingi ambazo sio za lazima na zinazoepukika. Ili kulinda maslahi ya pande zote mbili (muuzaji na mnunuzi), ni muhimu kuandaa mkataba wa mauziano kwa maandishi. Hii itasaidia kuepuka migogoro ya baadaye na kuhakikisha kuwa kila mtu anajua haki na wajibu wake.
Hapa kuna mwongozo wa jinsi ya kuandaa mkataba wa mauziano ya gari kwa usalama
1. Andika Taarifa za Pande Zote Mbili
Anza kwa kuweka taarifa kamili za muuzaji na mnunuzi:
- Majina kamili
- Namba za kitambulisho (NIDA, leseni ya udereva, au pasi ya kusafiria)
- Anuani kamili
- Namba za simu
Hii itawezesha mawasiliano ya baadae na kuthibitisha utambulisho wa kila upande
2. Maelezo ya Gari
Hakuna mkataba wa gari bila taarifa sahihi za gari husika. Hakikisha unataja:
- Aina ya gari (mfano: Toyota Premio)
- Modeli na mwaka wa kutengenezwa
- Namba ya usajili (plate number)
- Chassis number na namba ya injini
- Kilomita
- Rangi ya Gari
Taarifa hizi zitasaidia kuthibitisha gari linalohusika kwenye mkataba.
3. Bei ya Mauzo na Namna ya Malipo
Eleza wazi bei ya gari na namna ya malipo:
- Bei kamili ya gari
- Kiasi cha awali kilicholipwa (kama kuna advance payment)
- Salio linalobaki na tarehe ya mwisho ya malipo (kwa mauzo ya awamu)
- Njia ya malipo (cash, bank transfer, etc.)
Kwa malipo ya awamu, hakikisha unaweka ratiba ya malipo.
4. Tarehe ya Makabidhiano ya Gari
Eleza tarehe ambayo gari litakabidhiwa rasmi kwa mnunuzi. Pia, weka masharti kama mnunuzi ataondoka nalo siku hiyohiyo au baada ya kukamilisha malipo yote.
5. Hali ya Gari
Andika maelezo mafupi kuhusu hali ya gari kwa sasa. Mfano:
- “Gari linauzwa kama lilivyo (as-is condition).”
- Eleza kama kuna kasoro unazozijua (mfano: tairi limechakaa, au AC haifanyi kazi).
Hii itasaidia kuepuka madai ya baadaye kwamba gari lilikuwa na matatizo yaliyofichwa.
6. Masharti Muhimu ya Mauzo
Hakikisha mkataba unahusisha mambo haya:
- Gari linauzwa bila kudhaminiwa (no warranty) isipokuwa kama umekubaliana vingine.
- Mnunuzi atawajibika kwa uhamisho wa jina (ownership transfer) kwenye mamlaka ya usajili wa magari.
- Mnunuzi atawajibika kwa bima na kodi yoyote ya baadaye.
7. Saini na Mashahidi
Mwisho, pande zote mbili lazima zisaini mkataba mbele ya mashahidi wawili au zaidi. Mashahidi nao wasaini na waweke maelezo yao (jina na namba za kitambulisho).
Kama unaweza, ni bora mkataba upitiwe au uthibitishwe na mwanasheria.
8. Nakala za Mkataba
Toa nakala mbili au zaidi za mkataba. Muuzaji na mnunuzi kila mmoja apate nakala yake kwa kumbukumbu.
Hitimisho
Kuandaa mkataba wa mauzo ya gari si jambo la kupuuzia na jepesi. Mkataba mzuri ni kinga dhidi ya migogoro ya baadae. Hakikisha unaweka kila kitu kwa maandishi, uwe wazi na uwe mkweli. Kama huna uhakika, usisite kumshirikisha mwanasheria kwa ushauri wa