Hakuna kitu kizuri katika biashara kama pale unapouza kitu chako basi akapatikana mteja kwa haraka na akalinunua furaha yake sio ya nchi hii,lakini mambo yanakuwa magumu pake ambapo gari limechukua muda mrefu tokea litanganazwe kuuza na hakijauzika hali hii huwavunja moyo muuzaji na hakuna anayekupigia simu wala kuulizia. Hali hii ni ya kawaida katika biaashara, hasa kama kuna ushindani mkubwa au bei yako ni kubwa sana badala ya kusubiri tu, kuna hatua muhimu unazoweza kuchukua kuongeza nafasi ya kuuza gari lako haraka.
1. Angalia Bei Yako
Mara nyingi sababu kubwa ya gari kutopata wateja haraka ni bei kuwa juu kuliko thamani ya gari yenyewe na bei kwenye soko. Angalia magari yanayofanana na yako ambayo yanauzwa sehemu tofauti tofauti na hali inayofanana na lako, magari hayo unaweza kuangalia katika mitandao ya kijamii au tovuti kama garipesa.com, kisha linganisha bei. Kama bei yako ni ya juu sana, fikiria kupunguza kidogo ili kuvutia wateja
2. Piga Picha nzuri za Tangazo
Wateja wengi huangalia picha kabla ya kusoma maelezo. Hakikisha unapiga picha nzuri na unaweka picha nzuri, safi na zenye mwanga mzuri. Piga picha gari likiwa limeoshwa vizuri, onyesha sehemu muhimu kama injini, ndani ya gari, matairi na dashboard. Usitumie picha za zamani au zenye giza.
3. Weka Maelezo Yanayojitosheleza
Katika tangazo lako weka maelezo yanayojitosheleza kuhusiana na hilo gari kama vile hali ya gari, uzima wa gari, km ilizotembea, mwaka wa kutengenezwa nk. Eleza vitu vya ziada vilivyomo katika gari lako kama vile openroof, matairi mapya, mziki mkubwa, nk. Epuka kuweka maelezo mafupi sana kama “Gari linauzwa halina kipengere.”
4. Angalia Njia Za Kutangaza
Unapotaka kutangaza kuhusu kuuza gari lako sehemu ya kutangazia ni moja ya njia muhimu kwaajili ya kupata matokeo ya haraka sasa angalia wapi unaweka tangazo lako. Jaribu kuweka tangazo kwenye majukwaa mengi zaidi na yenye watu wengi, kama WhatsApp Status, Instagram, magroup ya Facebook ya magari, au hata kufunga karatasi ya FOR SALE kwenye gari lenyewe na kulibandika nyuma.
5. Fanya Marekebisho madogomadogo na Usafi
Wateja wakija kuangalia gari na kulikuta ni chafu au lina harufu mbaya, wanaweza kuwa na mawazo hasi kuhusiana na hilo gari. Fanya interior detailing, badili oil kama muda umefika, na kama kuna mikwaruzo inayoweza kutoka au kioo kibovu, rekebisha vile ambavyo ni vidogo vidogo. Hata marekebisho madogo yanaweza kufanya gari lionekane bora zaidi.
6. Weka Ofa
Unaweza kusema “Price Slightly Negotiable” au “Free Full Tank for the Buyer” ili kuwapa wanunuzi motisha ya kufika kukagua gari. Wengine hupenda kuona kuna nafasi yakubageini bei.
7. Fikiria Madalali
Kama unahisi kuwa kuuza wewe mwenyewe kunaweza kukucheleweshea kupata wateja basi fikiria kutafuta madalali na uwaeleze kuhusu gari lako na pia kama wanaweza kulipiga picha vizuri wafanye hivyo na kulitangaza lakini pia unaweza kulipeleka kwenye yards au kuwaachia madalali wanaojua mbinu za kuuza haraka. Ila hakikisha unakubaliana vizuri kuhusu malipo yao kabla.
8. Jipe Subira
Gari sio nyanya kusema mtu anafika anatoa hela anaondoka gari linahitaji umakini ukizingatia hio ni pesa ndefu sana inayotoka hapo mpaka mteja aamue kununua maana yake inachukua muda kwahio subira inahitajika sana na wakati mwingine soko linakuwa lipo chini kwa sababu ya kipindi fulani kama vile miezi ya kulipa ada. Usikate tamaa, badala yake endelea kujiuliza: “Ninawezaje kuboresha zaidi?” Rekebisha bei, badilisha picha, ongeza matangazo na kuwa mvumilivu.
Kwa kufuata hatua hizi, utaongeza nafasi yako ya kupata mnunuzi sahihi kwa bei inayokufaa.